Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa haukuwa na sababu ya kufanya usajili mkubwa wakati wa dirisha dogo la usajili.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wasingefanya usajili kwa kuwa kulikuwa na wachezaji wengi majeruhi ambao walikuwa wanarejea kundini.
"Ukiangalia wachezaji wengi ndiyo walikuwa wanarejea kundini wakitoka kujiuguza. Sasa hauwezi kufanya usajili mkubwa badala yake kuhakikisha wanapona.
"Baada ya hapo, tutaanza kuangalia perfomance (utendaji), mbele huko tutajua kama tunapaswa kuongeza wachezaji au la," alisema.
Yanga ilisajili wachezaji wawili tu akiwemo kinda Yohana Mkomola na usajili wake haukuwa na zaidi ya hapo.
Wachezaji wengi wakongwe wa Yanga walikuwa majeruhi kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi lakini Yanga wana furaha kwa kuwa wote wameanza mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment