Kiungo Haruna Niyonzima wa Simba amerejea na kuanza mazoezi mepesi baada ya kukaa kwa takribani wiki moja akijiuguza majeraha.
Niyonzima alipewa ruhusa ya kurejea kwao Rwanda kutokana na matatizo ya kifamilia kabla ya kurejea nchini.
Hata hivyo, kwa takribani wiki moja alishindwa kufanya mazoezi kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini leo, ameanza kujifua na Simba iliyokuwa inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam.
Kiungo huyo Mnyarwanda alikuwa akifanya mazoezi pembeni, akizunguka taratibu ikionekana ni maelekezo ya daktari kuanza mazoezi taratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment