Mkazi wa jiji la Tabora Miraji Shabani Misigaro(49) amekuwa mshindi wa 44 wa promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA inayoendeshwa na kampuni ya SportPesa Tanzania.
Miraji Shabani Misigaro ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza nafaka sokoni Tabora alisema "Shughuli zangu kama mnavyoniona mimi ni mjasiriamali ninayejishughulisha na biashara ndogo ndogo, lakini niliamua kujaribu bahati yangu kupitia kampuni ya SportPesa na kama mnavyoona sasa hivi vyuma vimeachia."
"Mama(mke wake) anajishughulisha na shughuli za kilimo na kwa muda huu yuko shamba na baadhi ya mavuno anayoyapata ndio tunatumia kufanyia biashara. Niliijua kampuni ya SportPesa hasa baada ya kuidhamini timu ya Everton kutoka Uingereza na kuja nchini hapa na ilinivutia na kama hivi nilijaribu na nimeshinda, bajaji hii itanisaidia kuendesha kipato changu"
Akizungumza juu ya ushindi wa baba yake Athumani Miraji alisema`'hakuwa anatushirikisha sana kwenye mambo yake ila baada ya kushinda alitupa habari, kwa leo hivi nimethibitisha kwamba ni kweli kwa mimi kama mm nimethibitisha kwamba baba atajiendeleza kuinua kipato chake kwa sababu usafiri mkubwa tulionao sisi ni baiskeli"
Kwa upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Utekelezaji na Utawala Tarimba Abbas aliongeza" Tumefurahi sana kupata mshindi wa kwanza kutoka Tabora ambaye amejinyakulia bajaji aina ya TVS KING DELUXE, hii inaonyesha jinsi gani watanzania kutoka sehemu mbali mbali ya nchi wanavyonufaika na hii promosheni.
Kushiriki kwenye promosheni hii ni rahisi,kwanza kabisa jisajiri kwa kutuma neno GAME kwenda 15888,weka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa kuweka kumbukumbu namba 150888 na 888 kama namba ya kampuni, weka ubashiri wako kisha tuma neno SHINDA kwenda namba 15888 baada ya hapo moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye droo itakayokupelekea wewe kushinda bajaji aina ya TVS KING DELUXE, Jezi Orijino ya moja kati ya timu tunazodhamini pamoja na safari ya kwenda Uingereza kushuhudia moja ya mechi zinazoshiriki ligi kuu" alimaliza Ndugu Tarimba.
0 COMMENTS:
Post a Comment