Mwanachama maarufu wa Yanga, Ibrahim Akilimali amesema anajiandaa kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akilimali ameiambia SALEHJEMBE, kwamba bado hajaamua lakini ni jambo alilokuwa analifikiria kuwania ubunge katika jimbo la Kinondoni.
“Hili ni jambo ambalo nimelifikiria, lakini si jambo ambalo tayari nimetangaza au kuchukua uamuzi wa kulifanya,” alisema.
“Ikifikia kama nimefikia uamuzi, basi nitatangaza rasmi lakini kwa sasa bado.”
Akilimali amekuwa kati ya sehemu ya viongozi wa wazee wa Yanga ingawa wamekuwa hawatambuliki kikatiba ya klabu hiyo.
Hata hivyo, hakueleza lini atakuwa tayari kuweka mambo hadharani kuhusiana ana uamuzi wake huo wa kugombea ubunge.
0 COMMENTS:
Post a Comment