December 13, 2017



Huku michuano ya Kombe la Chalenji ikitarajiwa kuanza hatua ya nusu fainali kesho Alhamisi, tayari Simba imemnasa straika wa Zanzibar Heroes, Kassim Khamis na inafanya juhudi za kutaka kumsajili katika usajili huu wa dirisha dogo unaofungwa keshokutwa Ijumaa.

Straika huyo anayeitumikia Klabu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya, amecheza mechi mbili pekee kwenye mashindano hayo kabla ya kuumia na kukosa mechi mbili zingine. Katika mechi hizo alizocheza, amefunga mabao mawili dhidi ya Rwanda na Kilimanjaro Stars.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, alisema katika kufuatilia kwake michuano hiyo, kwa wachezaji wazawa amemuona straika huyo pekee ndiye mwenye nafasi ya kujiunga na Simba.

“Wachezaji wengi ni wazuri lakini huwezi kuwasajili wote, lazima uchague kulingana na mahitaji ya kikosi chako. Kwa upande wangu naweza kusema yule straika wa Zanzibar ambaye aliwafunga Rwanda na Tanzania Bara (Kassim Khamis Selemani) ndiye anayetufaa, ni vyema tukamsajili,” alisema Djuma.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic