TSHISHIMBI MAZOEZINI YANGA LEO. |
Kiungo mkabaji wa Yanga Mkongo, Papy Kabamba leo ameruhusiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake ya kuchezea mpira.
Hiyo, ni baada ya kiungo huyo kumaliza program ya mazoezi mepesi ya binafsi juzi Jumatano.
Kiungo huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili na nusu kutokana na majeraha ya enka.
Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavu alisema amemruhusu kiungo huyo kuchezea mpira baada ya kuwa fiti, hivyo mechi dhidi ya Polisi Tanzania upo uwezekano wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment