Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameendelea na mazoezi leo baada ya mapumziko ya siku moja.
Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake chini ya Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa.
Nsajigwa anashika majukumu ya Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye amesafiri kurejea kwao Zambia kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanaye aliyehitimu masomo.
Yanga inajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania ambayo sasa itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa Jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment