December 22, 2017







Ile Madini iliyowahi kuisumbua Simba katika michuano ya Kombe la Shirikisho, wamekutana na kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Ruvu Shooting.

Madini, walianza kupata bao kupitia John Kizule lakini baada ya hapo walianza kushambuliwa mfululizo na Hamis Mcha akafunga bao la kusawazisha kwa mkwaju wa faulo.

Dakika ya 35, Mcha maarufu kama Vialli akafunga bao la pili na dakika tatu baadaye, Shala Juma akafunga bao la tatu kwa Shooting.


Vialli alifunga bao la nne katika dakika ya 60 na kuhitimisha huku akifunga hat trick yake ambayo ni ya kwanza katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic