January 20, 2018

KIKOSI CHA AFRICAN LYON KILICHOKUWA LIGI KUU BARA MSIMU ULIOPITA

Uongozi wa African Lyon, umeipongeza JKT Ruvu iliyoifunga timu hiyo kwa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza.

Ushindi huo umeihakikishia JKT Ruvu kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika barua iliyoandikwa na Mkuu wa Benchi la Ufundi la African Lyon, Charles Otieno imeeleza namna ambavyo ilifungwa kwa soka safi na la juhudi la JKT na kuwapa pongezi.

“Tunakubaliana na kufungwa kwa kuwa ni matokeo ya mpira, tunawaomba radhi mashabiki wetu na kuwaahi kuwa tutajituma zaidi kupambana.


“Lakini tunawapongeza JKT pamoja na kuwa walionekana wameishapanda lakini walicheza kwa juhudi kubwa,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic