January 26, 2018



Kocha Mkuu wa Yanga, amewaandaa Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu ili kuimaliza Azam leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azma Complex jijini Dar.

Yanga katika mazoezi yao ya mwisho leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, Lwandamina aliwakuwa akiwanoa vijana wake huku akionekana kukiandaa kikosi kitakachoanza kesho.

Katika mazoezi hayo, kikosi ambacho kinaonekana kitaanza kesho, kipo hivi; Rostand Youthe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Raphael Daud, Said Makapu, Emmanuel Martin, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa.


Lwandamina ambaye alikuwa akiwaongoza vijana wake huku leo akitarajiwa kukaa katika benchi baada ya kibali chake cha kazi kuwa safi, alikuwa akiwafundisha katika kutumia mifumo mitatu ambayo 4-4-2, 4-3-3 na 3-5-2 huku vijana wake hao wakionekana kuelewa haraka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic