January 26, 2018




Yanga kesho Jumamosi itacheza dhidi ya Azam bila ya nyota wake saba ambao wansumbuliwa na majeraha, huku mmoja akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Wachezaji hao ni Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Yohana Nkomola, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Donald Ngoma.

 Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema: “Tutawakosa nyota saba katika mchezo wetu wa kesho dhidi ya Azam, lakini wengine wapo tayari kwa mchezo huo ambao ni lazima tuibuke na ushindi ili tuwe kwenye nafasi nzuri katika msimamo.

“Buswita licha ya kuwa na adhabu ya kuukosa mchezo huo kutokana na kutumikia kadi tatu za njano, lakini pia ni majeruhi kama walivyo hao wengine sita.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic