January 25, 2018



Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi yake chini ya Kocha mpya, Pierre Lechantre. Lakini mwonekano mpya wa mshambuliaji Emmanuel Okwi, umekuwa gumzo.

Okwi ambaye ni kinara wa upachikaji mabao Ligi Kuu Bara kwa sasa, aliibuka kwa mara ya kwanza akiwa amenyoa tofauti na muonekano mpya wa kipara au “dongo”.

Mganda huyo alishiriki mazoezi vilivyo lakini mashabiki walikuwa wakizungumza mwonekano wake huo wa dongo kabla ya Simba kuivaa Majimaji.


Lechantre raia wa Ufaransa, ameiongoza Simba siku yake ya pili kazini akisaidiwa na wasaidizi wawili, Masoud Djuma na Mohamed Habibi.

Kwa siku ya pili mfululizo mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic