January 25, 2018


Kiungo anayechipukia kwa kasi wa Yanga, Pius Buswita ametokea katika mazoezi ya timu hiyo na kuwaoa moyo wenzake wenye kazi ya kuhakikisha wanachukua pointi tatu dhidi ya Azam FC.

Yanga itaivaa Azam FC keshokutwa Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Buswita alikuwa mazoezini kuungana na wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru ambako walikuwa wakijitoa kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Azam FC inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Lakini Buswita aliyefunga bao la ushindi katika mechi iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting, ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic