January 25, 2018


Mashabiki wa Simba wameanza kujitokeza kwa wingi wakionyesha wazi kwamba wanataka kuona kazi ya makocha wao wapya wakishirikiana na msaidizi Masoud Djuma inakuwaje.

Makocha wapya, Pierre Lechantre ambaye ni kocha mkuu raia wa Ufaransa na msaidizi mwingine, Mohamed Habibi walianza kazi rasmi jana.

Mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam kuwashuhudia.

Mashabiki hao walikuwa kimya muda mwingi wakiangalia kilichokuwa kikitolewa na makocha hao.


Baada ya mazoezi, mashabiki wengi walionekana kufurahishwa na mambo yalivyokwenda huku baadhi wakitaka subira ivutwe ili kuangalia mambo yatakavyokuwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic