January 25, 2018


Kocha wa Viungo wa Simba, Mohamed Habibi raia wa Tunisia anaonekana kuanza kazi yake kuongeza nguvu na kasi katika kikosi chake,

Kocha huyo ni mmoja wa makocha wawili wasaidizi wa Simba, mwingine ni Masoud Djuma wote wakiwa chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.

Habibi ameanza kazi yake jana kwa mazoezi ya taratibu lakini yanayoonyesha kutaka kujenga ufiti wa wachezaji wake kwa kiwango cha juu.

Kuonyesha kwamba anaijua vizuri kazi yake, Habibi alikuwa akifanya mazoezi yanayoonekana kuwa ni laini lakini mwisho wachezaji walichoka.

Baadaye alisema hatafanya mazoezi makali kwa kuwa timu iko katika ligi na hakuna muda mrefu wa kufanya mazoezi makali. Lakini akasisitiza kupitia mazoezi hayo watakuwa wakiimarika.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic