January 29, 2018



Kicha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amemchagua kiungo wake, Papy Tshishimbi na beki wa Azam, Bruce Kangwa kuwa ndiyo wachezaji bora wa mechi ya juzi Jumamosi wakati timu hizo zilipopambana.

Juzi Jumamosi, Azam ilikuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar na kushuhudiwa Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo, Azam ilianza kufunga bao kupitia kwa Shaban Idd, kabla ya Obrey Chirwa na Gadiel Michael hawajaifungia Yanga mabao yaliyowapa ushindi.

Akizungumzia viwango vya wachezaji kwenye mchezo huo, Lwandamina amesema: “Ningeweza kusema mchezaji bora wa mechi ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, lakini ile kadi nyekundu imemuharibia, hivyo basi Tshishimbi na Kangwa hao kwangu ndiyo walikuwa bora kwa muda wote wa mchezo.”


Ikumbukwe kuwa, Kangwa raia wa Zimbabwe ndiye aliyetengeneza bao pekee kwa Azam, huku Tshishimbi akijenga ngome imara ya kiungo akishirikiana na Said Juma Makapu na Raphael Daud.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic