January 29, 2018



Kocha Arsene Wenger, amekubali kumtwaa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubamenyang kwa dau la pauni milioni 55.4.

Dau hilo litakuwa ni rekodi mpya ya usajili wa Arsenal kwa mshambuliaji huyo kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Iwapo Aubameyanga raia wa Gabon atatua Arsenal, atakuwa akichukua mshahara wa pauni 180,000 kwa wiki.

Taarifa zinaeleza, Dortmund wameanza mazozungumza na Chelsea ili kumsajili mshambuliaji Michy Batshuay baada ya suala la kumsajili Olviere Giroud kukwama kutokana na familia ya Mfaransa huyo kusisitiza inataka kubaki London.


Chelsea wakati wanajua Batshuay atakwenda Dortmund, wao wako katika hatua za mwisho kuongeza washambulizi wawili ambao ni Edin Dzeko na Emerson kutoka AS Roma ya Italia.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic