January 3, 2018


Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa ameonyesha kweli yuko vizuri baada ya kufunga bao katika mechi yake ya kwanza akiwa amerejea kuichezea timu hiyo baada ya kuondoka Chelsea.

Atletico Madrid kwa mabao 4-0 katika mechi ya michuano ya Copa del Rey dhidi ya Lleida.

Costa amefanikiwa kufunga bao dakika tano tu baada ya kuingia uwanjani, lakini bahati mbaya akajiumiza mwenyewe wakati akishangilia na kutolewa nje kupata matibabu, hakurudi uwanjani.

Pamoja na yeye kufunga, washambulizi wengine wa Atletico, Antoine Griezmann na Fernando Torres nao kila mmoja alifunga bao.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic