January 2, 2018



Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini nayo imeingia katika vita ya kumtwaa mshambuliaji Elius Maguri.

Taarifa za uhakika zinaeleza, Cape Town City imefanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo ambaye pia bado anawaniwa na Difaa Al Jadid ya Morocco anayoicheza Saimon Msuva.

Awali ilielezwa anaweza kujiunga na timu nyingine ya Afrika Kusini lakini sasa Cape Town City ambayo inajiimarisha inaonyesha nayo imeingia katika mbio hizo.

Mazungumzo kati ya wakala wa Maguri na Difaa yanaonekana kwenda vizuri na kama yatakaa sawa, anaweza kujiunga nayo.


“Kweli kumekuwa na mazungumzo na yanakwenda vizuri sana. Hapo limebaki suala la maslahi,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic