January 2, 2018




Tayari kuna timu kadhaa za Afrika Kusini na Morocco zimeonyesha nia ya kumtwaa mshambulizi, Habibu Kiyombo wa Mbao FC.

Hii inatokana na mabao yake matatu aliyofunga katika mechi za Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga na Simba.

Tayari mmoja wa mawakala walio fasta ametuma video za mabao hayo matatu na anasema, inaonekana wamevutiwa ingawa kuna ugumu wa kutoa fedha.

“Nimetuma video zake, unajua nilianza kumfutilia baada ya kuifunga Simba bao zuri sana walipotoka 2-2. Lakini nimeona amerudia kufunga bao lenye ubora uleule.

“Kazi yangu ni kuhakikisha Tanzania ina wachezaji wengi wa kulipwa na nimekuwa nikifanya hivyo kwa kuwafuatilia wachezaji wengi,” alisema wakala huyo ambaye kaishawapeleka wachezaji kadhaa maarufu wa Tanzania na wengine wanacheza nje.

“Kama wataridhika naye na watakuwa na ofa nzuri, basi moja kwa moja nitaanza kuwasiliana na Mbao FC ili kumpa nafasi ya kwenda nje,” alisema.

Hata hivyo, wakala huyo hakutaka kuandikwa akidai angependa kufanya mambo yake kimyakimya hadi yatakapofikia wakati sahihi..


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic