February 15, 2018


MPIRA UMEKWISHAAAAAAA

-KADI Sangija analambwa kadi ya njano kwa kuzuia mpira haujapigwa
-Krosi ya Kichuya, mpira unaokowa na kuwa kona, inachongwa, haina manufaa


DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
KADI Dk 90 Mobi analambwa kadi ya njano 
GOOOOOOOOOOO Dk 89 Nonga anaunganisha vizuri mpira wa faulo na kumshinda Manula 
Dk SUB Dk 87 Simba wanamtoa Mavugo aliyeingia na nafasi yake inachukuliwa na Bukaba kuongeza ulinzi 


KADI Dk 84, Juuko analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa NYEKUDNU
Dk 84, Kichuya anaachia mkwaju wa adhabu lakini Massawe anazidi kuonyesha yuko vizuri
Dk 83, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa MWadui wanaonekana wako kwenye shepu ya kusawazisha
Dk 80 shuti jingine kali karibu na lango la Simba, goal kick
Dk 77, kipa anapangua shuti la Mavugo ilikuwa karibu kabisa
KADI Dk 75, Awesu analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha
Dk 73 Awesu anaingia vizuri katika eneo la 18 lakini anajiangusha na mwamuzia namuambia acha ujanja
GOOOOOOOOOOOO Dk 71, kwa mkwaju wa penalti Okwi anaandika bao la pili la Simba, bao la kwaza kwake la mkoani


KADI DK 70 Mgeveke anainuka na kulambwa kadi ya njano
PENAAAAAT Dk 67, Mgeveke anamuangusha Okwi ndani ya 18, wote wawili wako chini
Dk 65, piganikupige kwenye lango la Mwadui lakini Mobi anaondosha
Dk 64, Massawe anafanya kazi ya ziada na kuokoa, inakuwa ni kona
SUB Dk 64 Nicholas Gyan anaingia kuchukua nafasi ya Ndemla
KADI Dk 63 Kipa Massawe, analambwa kadi ya njano baada ya kuda nje ya 18
KADI Dk 61, Juuko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sheva au Miraji
GOOOOOOOOO Dk 59 Luhende anafunga bao safi kabisa kwa mkwaju wa adhabu



Dk 58, MWadui FC wanapata faulo nje kidogo ya 18 ya Simba, ni sehemu mbaya hii
Dk 54, MWadui FC wanaonekana kuizidi Simba katika eneo la katikati ya uwanja
Dk 50 Mwadui FC wanaendelea kushambulia kwa kasi, wanapata kona, inachongwa na Awesu, ilikuwa hatari, lakini Juuko anaokoa unakuwa kurushwa
Dk 47, Mwadui wanaonekana wameanza vizuri wakiongozwa na Awesu wametawala eneo la katikati ya uwanja
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi, MWadui wanaonekana wanataka kupata bao la kusawazisha



MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa, kipa anadaka
Dk 43, mwamuzi amesimamisha mpira ili wapate mapumziko mafupi ya maji
Dk 41, nje ya 18, Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali kabisa, unapita juu kidogo ya lango la Simba
Dk 38 Simba wanapata kona nyingine, inachingwa vizuri kabisa lakini goal kick
Dk 36 Okwi anageuka vizuri, anapiga chenga na kuachia mkwaju maridadi, lakini anaokoa vziuri kabisa
Dk 32 Zimbwe anatoa boko, Miraji yeye na kipa Manula, anaokoa
Dk 31, mpira wa juu kwenye lango la Simba, anaruka juu Manula, goal kick
SUB Dk 29 Mavugo anaingia kuchukua nafasi ya Bocco aliyeumia


KADI Dk 27, Zimbwe analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 26, Mwadui FC wanaonekana kuwa na haraka maana wanapoteza pasi nyingi sana
Dk 22, krosi safi ya Ndemla katikati ya lango mpira unapita bila mwenyewe, mabeki na washambuliaji wanaukosa
Dk 21, mpira safi wa kona wa Ndemla, Kotei anauwahi lakini Mobi anaondosha vizuri kabisa


Dk 20, kipa Massawe anafanya kazi nyingine ya ziada kupangua shuti la Ndemla na kuwa kona
Dk 19, Kichuya anapiga kona fupi kwa Kapombe lakini Luhende anawahi na kuondosha
Dk 18, Okwi akitokea kidogo anaachia krosi lakini beki Mwadui anatoa na kuwa kona
Dk 17, Zimbwe anaingia vizuri pembeni, anaachia krosi lakini kipa Massawe anawahi na kudaka
Dk 15, Kichuya anaachia mkwaju wa kuzungusha, kipa Masawa anadaka vizuri kabisa
Dk 14, Okwi anamtoka Mobi lakini anatoa inakuwa kona, inachongwa, inaokolewa
Dk 12, inachongwa kona hapa, Luhenda anaondosha vizuri kabisa


Dk 11 Kapombe anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali kabisa, kipa anafanya kazi ya ziada anapangua na kuwa kona
GOOOOOOO Dk 9, Bocco anauwahi mpira na kupiga kichwa safi, anaandika bao la kwanza
Dk 7 sasa, bado mpira haujachangamka sana na inaonekana MWadui wanacheza zaidi upande wa lango lao
Dk 5, Simba wanaingia vizuri, pasi nzuri ya Ndemla lakini mpira unampita, MWadui FC wanaokoa
Dk 3, Mwadui FC nao wanafika katika lango la Simba lakini mpira mrefu wa Luhende unakosa mwenyewe
Dk 1, mechi imeanza na Simba wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui FC, wako makini







1 COMMENTS:

  1. Simba hawakutumia vizuri nafasi zilizopatikana kipindi cha kwanza. Wachezaji hasa baada ya kutoka John Bocco kama vile walirelax hawakujituma sana. Binafsi sikuona nguvu yeyote kwa mafowadi. Mpira ungeendelea Mwadui wangeweza kupata goli la 3. Simba wachezaji wanajisahau sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic