Wachezaji wa Yanga na benchi zima la ufundi watafika nyumbani kwa nahodha wao, Nadir Haroud Cannavaro kumpa pole kutokana na msiba uliomkuta.
Cannavaro amekutwa na msiba wa kufiwa na mwanaye ambaye amezikwa jana jijini Dar es Salaam.
Wakati msiba unatokea, Yanga walikuwa nchini Shelisheli wakipambana na St Louis ambako walipata sare ya bao 1-1 na kusonga mbele.
Kikosi cha Yanga kimerejea usiku wa jana na leo kimeendelea na mazoezi asubuhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment