March 6, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford, amesema hajawahi kuhusika na urejeo ambao uliiwezesha timu yake kupata matokeo dhidi ya Crystal Palace 'Come Back' katika mchezo wa jana zaidi ya kutazama kwenye TV.

United ilirejea kipindi cha pili na kuweza kuchomoa mabao mawili kisha kuongeza la 3 na kufanya mchezo huo umalizike kwa mabao 3-2.

Palace walianza kufunga kipindi cha kwanza katika dakika ya 11 kupitia Townsend na kisha baadaye Aanholt akafunga dakika ya 48, kalbla ya Smalling kufunga la kwanza kwa United dakika ya 55.




Baadaye Lukaku alifunga dakika ya 76 kabla ya msumari wa mwisho kupigiliwa na Nemanja Matic dakika ya 91.

Matokeo hayo yaliirejesha United nafasi ya pili kwa kufikisha alama 62 dhidi ya Liverpool iliyoshika nafasi hiyo kwa muda ikiwa na alama 60.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic