March 8, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuhudhuria katika mtangange wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya Al Masry SC, Afisa Habari wa zamani wa Young Africans, Jerry Muro, amesema kuwa si vema ushabiki ukasababisha kuondoka kwa uzalendo.

Jerry ameamua kuwa mfano wa wadau wa Yanga waliojitoa kwenda kuipa hamasa Simba katika mchezo ambao timu hizo zimeenda sare ya mabao 2-2.

Na kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muro aliandika haya kwa uchache

JERRY MURO AKIWA NA MASHABIKI WA SIMBA KATIKA MCHEZO WA SIMBA
DHIDI YA AL MASRY, KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

6 COMMENTS:

  1. Jerry Muro amebadilika siku hizi anakuwa na mawazo mazuri ya mshikamano. Hongra Jerry

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwambieni na Yule mropokaji wenu nae abadilike

      Delete
  2. Wewe unamwita mropokaji, lakini mechi za mwanzo ambazo yanga alikitifua na st. Louis huku simba akimenyana na grandamarie manara alisisitiza hilo. Lakini upande was pili ukajibu hauhitaji kuishangiliwa na simba na hawataishangilia simba.

    ReplyDelete
  3. Siasa zimegoma tunarudi michezoni!
    Uzalendo ni vigumu kupatikana katika timu zetu kwa sababu bado zinacheza mpira vijiweni na kwenye media.
    Tukibadilika uzalendo kwenye michezo utakuja wenyewe na si kwa kiki na filimbi.

    ReplyDelete
  4. Haji alijaribu kuleta muafaka wavimba macho wenzako wakampinga. Kushangilia timu za nje ni tatizo lakini tatizo kubwa zaidi ni kujidhalilisha na kwenda kuomba jezi kama walivyofanya makomandoo wa Yebo Yebo. Sishangai sana kwani wamezoea kupiga magoti wakiomba fadhila .Lipeni mishahara man wadhamini 2 Sports pesa na Macron.Pesa zinakwenda wapi?Wachezaji miezi 4 hawajalipwa mishahara.

    ReplyDelete
  5. Waambie hao waache maneno, watimize wajibu wao. Walitamba wachezaji wakitoka Mtwara watajazwa mapesa, maana matajiri wao wameongea nao wanataka washinde ili wawalipe, vijana wamepigana kweli wakashinda, hadi sasa kimya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic