March 8, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Juventus imepindua matokeo katika dimba la Wembley baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.

Katika mchezo Tottenham walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 36 kupitia Son Heung, na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Tottenham walikuwa wanaongoza kwa bao hilo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Kibibi Kizee kujitutumua kupata matokeo, na katika dakika ya 64, Higuain alisawazishia Juventus na kuufanya mchezo huo uwe 1-1.

Kiungo Dybala aliondoa rasmi ndoto za Tottenham kuingia 8 bora ya michuano hiyo, baada ya kupigilia msumari wa pili kwa Juventus, ikiwa ni dakika ya 67 na kufanya idadi ya mabao kwa ujumla kuwa 3-4.

Mechi ya awali iliyopigwa Italy, ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2. Matokeo haya sasa yanaifanya Juventus kuungana pamoja na vilabu ya Liverpool, Real Madrid na Manchester City iliyofuzu pia.





Mbali na Juventus, Manchester City nao licha ya kufungwa mabao 2-1 na FC. Basel leo, wamesonga mbele mpaka robo fainali. 

Katika mechi ya awali City walishinda ugenini kwa jumla ya mabao 4-0, na sasa idadi kamili imekuwa ni mabao 5-2


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic