ASIKWAMBIE MTU, JINA LA BEN YEDDER NDIYO GUMZO HIVI SASA MITANDAONI
Jina la Ben Yedder limezidi kuteka vichwa watu kwa wadau wengi wa soka hapa Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla kufuatia mabao aliyofunga dhidi ya Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya usiku wa jana.
Yedder aliifungia Sevilla mabao hayo mawili kwenye dakika za 74 na 78, mabao yaliyoipa tiketi United ya kuaga rasmi safari ya kuendelea na mashindano hayo ikiwa ni hatua ya 16 bora.
Mfaransa huyu, Wissam Ben Yedder (27) amekuwa gumzo kubwa haswa kwa mashabiki ambao ni wapinzani wa United, si tu mashabiki, bali hata mitandao mbalimbali imekuwa ikiweka picha na habari zake.
Mabao yake ya jana yamewafanya baadhi ya mashabiki wa Liverpool kumtumia kama kipoozeo haswa baada ya majogoo hao kupoteza dhidi ya United katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu England.
Baada Yedder ya kuiwezesha Sevilla kuvuka hatua ya 16 bora, timu hiyo sasa imeungana na Real Madrid, Manchester City, Liverpool pamoja na Juventus kwenye hatua ya 8 bora ya mashindano hayo.








hahahha jana amenyoosha watu fulani hivi wanaongeeeeeeeeeeeea
ReplyDeletehttps://maisha360tz.blogspot.com/