March 17, 2018


Na George Mganga
 
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba Sc hautorushwa hewani na kituo chochote cha Runinga.

Awali kulikuwa na matarajio ya mechi kuoneshwa na kituo cha Azam TV baada ya kutangaza kurusha mechi ya Township Rollers dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema uongozi wa Al Masry umeigomea Azam TV kurusha mechi hiyo itakayoanza saa 2:30 usiku ambapo sababu hazijajulikana.

Saleh Jembe itakuletea kila litakalokuwa linajiri katika mchezo huo utakaopigwa Port Said Stadium, usiku wa leo. Endelea kuwa nasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic