KOCHA STAND UTD: SISI NI KAMA TOWNSHIP ROLLARS, TUPO TAYARI KUCHUKUA POINTI TATU LEO
Na George Mganga
Kocha wa Stand United, Athuman Bilal 'Bilo', baada ya kuwatambia Simba kwenye mchezo ambao walilazimisha sare ya mabao 3-3, leo amewaambia Yanga wajiandae kupoteza.
Bilo amesema wao ni sawa na Township Rollers ambayo iliifunga Yanga hapa nyumbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo wamekuja na tahadhari ya kuchukua alama tatu.
Akizungumza na ripota wa Saleh Jembe, Bilo ameeleza kuwa wamejiandaa vya kutosha kuelekea mchezo wa leo, huku akisema wanaijua Yanga ambayo ni ya kawaida wala haina makali yoyote.
"Sisi ni kama Township Rollers, tumejiandaa vya kutosha na wala hatuoni ukali wowote kutoka Yanga, tutapambana zaidi kubeba alama tatu leo" amesema Bilo.
Aidha Kocha huyo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kutoa hamasa kwa Stand United 'Chama la Wana' kutoa hamasa kwa wachezaji wa timu hiyo.








Acha maneno,chezeni mpira kama mlivyocheza na Simba.Msituletee za Maxime na Kagera Sugar yake.Mchezaji anasaidia kuongenza goli la tatu utafikiri wako kwenye mazoezi.Natamani hizi timu dizaini hii washuke daraja kama Toto wanaogawana magodoro ya klabu
ReplyDeleteila zile zinazofungwa hadi goli saba mfano Ruvu shooting zisishuke ili mikia wajipigie tu
Delete