March 11, 2018


Wakati Yanga ikiwa na kibarua cha kuivaa Stand United kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaa kesho, beki wa kulia, Juma Abdul, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kupitia ukurasa wa Facebook wa klabu hiyo, beki huyo amesisitiza akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho kuipa hamasa timu yao ili iweze kuibuka na ushindi huku akisema ubingwa unawezekana.

"Kikubwa ninaomba mashabiki wa Yanga wajitokeze katika mchezo wa kesho, uwepo wao unatupa hamasa ya sisi kupambana uwanjani. Ubingwa unawezekana, hakuna kukata tamaa" alisema Abdul

Yanga itakuwa ina kibarua dhidi ya Stand United, mechi ambayo kama Yanga itashinda itapunguza pengo la alama kuwa 3 dhidi ya Simba inayoongoza Ligi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic