MSUVA AENDELEA KUWA KIPUSA EL JADIDA, AFUNGA BAO PEKEE DHIDI YA AS VITA YA CONGO, LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Na George Mganga
Winga wa kimataifa kutoka Tanzania anayekipiga Difaâ Hassani El Jadida ya Morocco, jana ameendelea kuwa tegemeo kwa timu yake baada ya kufunga bao pekee dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika mchezo huo uliokuwa wa raundi ya kwanza, Msuva alifunga bao pekee dakika ya 8 na kuipa nafasi nzuri timu yake kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bao hilo kwa Msuva linakuwa la nne sasa kuafuatia kufunga mabao matatu 'Hattrick', katika mchezo uliopita dhidi ya Benfica Bissau kutoka Guinea Bissau.
Baada ya matokeo hayo, Difaâ Hassani El Jadida, watapaswa kwenda sare yeyote ama kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa baada ya siku 10 ama 11 mjini Kinshasa, Congo.
0 COMMENTS:
Post a Comment