Machi 17 Yanga itakuwa ugenini jijini Gaborone Botswana kuivaa Township Rollers ya nchini humo katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy amehoji "vipi washindwe kuwafunga kwa hata kama wako ugenini."
Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga ililala kwa mabao 2-1 na kuijfanya iwe na mlima mrefu wa kupanda.
Kessy amesema wanajiamini na Yanga ina uwezo wa kushinda mechi hiyo.
“Kama wao walitufunga hapa nyumbani kwetu kwa nini sisi tushindwe kuwafunga kwao? Tunakwenda kuwafunga kwao kwani ni timu ya kawaida, kikubwa tunaomba sapoti ya mashabiki.”
Mbali na Kessy, beki mwingine wa pembeni anayetokea kushoto, Gadiel Michael naye anaamini Yanga itafanya yake kwa kuwa watapambana hasa.
“Tulipoteza mechi ya hapa nyumbani kutokana na makosa madogo, tunafanya marekebisho tukawafunge kwao kwani baadhi ya majeruhi wamerudi."
Pamoja na kupoteza, Kessy na Gadiel walionyesha kiwango bomba katika mechi hiyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment