March 11, 2018





Yanga wanaamini wana nafasi ya kufanya kile kisichowezekana kule Botstwana.

Wengi wamekuwa na hofu kwamba watafungwa mabao mengi kutokana na kile kilichoonyeshwa na wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Town Rollers ya Botswana.

Katika mechi ya kwanza, licha ya kuwa nyumbani, Yanga ililala kwa mabao 2-1.

Bosi msaidizi wa benchi la ufundi la Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wanajiamini na watawashangaza wengi watakapokuwa ugenini.




Mechi hiyo ni Machi 17 jijini Gaborone na itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini humo.

Tayari viingilio viko hadharani kuwani Pula 40, sawa na Sh 9,240.


“Rollers siyo wazuri wa kufikia hatua ya kukata tamaa ya kufanya vizuri katika mchezo ujao wa marudiano, nikuhakikishie kuwa kama wachezaji wetu watacheza kwa kufuata maelekezo yetu vizuri, niamini tunakwenda kuwatoa nyumbani kwao.


“Wanayanga wanatakiwa kuendelea kutupa sapoti ili katika mechi hiyo ya marudiano tupate ushindi mzuri utakaotupeleka katika makundi, mashabiki hawataamini kitakachotokea.


“Katika mchezo uliopita, tulishindwa kuwadhibiti katika kiungo na tukawaacha wakatawala na kusababisha kupiga pasi nyingi, kitu ambacho tumekiona na tunakifanyia kazi kisijirudie,” alisema Nsajigwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic