March 15, 2018


Na George Mganga

Baada ya Chelsea kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya FC, Barcelona kwa jumla ya mabao 3-0, lawama zote zinatupiwa kwa mlinda mlango, Thibaut Courtois.

Kupitia mitandao mbalimbali mashabiki wengi wa Chelsea wamemuandama Golikipa huyo, wapo wengine wanasema amechoka na pengine aondoke klabuni hapo na akatafute maisha mahala pengine.

Courtois aliruhusu mabao matatu ya Lionel Messi aliyefunga mawili, pamoja na Oeusman Dembele aliyefunga moja na jumla kuwa 3-0.

Mabao aliyofungwa na Messi yamekuwa gumzo zaidi, kutokana na baadhi kudai Courtois angeweza kuokoa mipira hiyo iliyopita katikati ya miguu yake.

Kitendo cha kuruhusu mabao hayo kimekuwa kero kubwa kwa mashabiki wa Chelsea ambao timu yao ishatolewa rasmi kwenye mashindano.

Baada ya Barcelona kufuzu kuingia robo fainali, droo ya timu zitakazokutana kwenye hatua hiyo inataraji kupangwa kesho.

Timu zilizofuzu ni Liverpool, Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, AS Roma, Sevilla, Juventus na FC. Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic