March 14, 2018



Kocha Msaidizi wa Stand United, Athumani Bilali ‘Bilo’ amewatupia lawama waamuzi waliochezesha mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Katika mechi hiyo, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 na kufanikiwa kuifikia Simba katika idadi ya pointi ikiwa na 46.

Bilo alisema makosa ya waamuzi akiongozwa na mwamuzi wa kati, Salim Singano kutoka Tanga ndiyo yaliwagharimu kusababisha kupoteza mchezo huo.

Bilo alisema, kitendo cha mwamuzi msaidizi namba moja Anold Bugando wa Singida kuinua juu kibendera wakati bao la kwanza likifungwa na Yusuph Mhilu baadaye akakishusha na mwamuzi wa kati akikubali bao hilo ndiyo kiliwapunguza morali.
“Tumepoteza mchezo kwa nguvu za waamuzi kwa sababu waliisaidia timu pinzani kwa makosa madogomadogo ya hapa na pale, bao la kwanza wakati linafungwa line one ananyoosha kibendera wachezaji wangu wakasimama Yanga wakafunga.
“Waamuzi waliochezesha mchezo wetu dhidi ya Yanga mimi binafsi sijawafurahia, wao ndiyo wamesababisha sisi tufungwe mabao hayo ambayo ni mengi,” alisema Bilo.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic