HAJI MANARA MANARA ANA OMBI HILI KWA MASHABIKI WA SIMBA KUELEKEA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO
Na George Mganga
Afisa Habari wa klabu ya Simba, haji Manara, amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mechi ya kesho.
Simba itakuwa inacheza mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry kutoka Egypt katika Uwanja wa Taifa, mchezo ukianza saa 12 kamili jioni.
Manara ameeleza kuwa anatambua mchango wa mashabiki hivyo vema wakaja kwa wingi uwanjani ili kuipa hamasa timu na wachezaji kwa ujumla.
Aidha Manara amewaomba mashabiki wazidi kununua tiketi kwa wingi ili wapate urahisi wa kuweza kutazama mechi hiyo Jumatano hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment