LICHA YA KUONDOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO, SIMBA WAMWAGIWA SIFA KEDEKEDE NA WAMISRI
Na George Mganga
Baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho jana Jumamosi, mashabiki wa Al Masry wameipongeza timu hiyo kwa kuonesha kiwango kizuri.
Mashabiki wengi hao walishangazwa na kiwango ambacho kilipelekea mechi hiyo kwenda suluhu ya 0-0.
Isitoshe pia, baadhi walisema kulikuwa na uwezekano wa kupoteza mchezo huo kulingana na namna Simba walivyokuwa wanakuja juu kulishambulia lango la Al Masry.
Baadhi ya mashabiki waliozungumza na Global TV, walitoa pongezi hizo kwa wachezaji wa Simba kwa namna walivyofanya mechi hiyo kuwa na matokeo tofauti na walivyitarajia.
Simba imeondolewa na Al Masry kutokana na faida ya bao la ugenini, na hii ni baada ya mchezo wa mkondo wa awali kwenda sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.
Miaka yote timu zetu zikipigwa Misri huwa zinamwagiwa sifa.
ReplyDeleteIla cha msingi hatuhitaji sifa tunahitaji kusonga mbele.