March 17, 2018









Na mpira umekwisha, dakika 4 za kipindi cha pili zimemalizika, Yanga wanaondolewa kwenye mashindano baada ya mechi ya awali kukubali kipigo cha mabao 2-1/

Dk 93, Mabadiliko mengine Rollers wanafanya.
Dk 91, Ajib na mpira, anapiga chenga mabeki wa Rollers, anadonoa shuti lakini mabeki wanaokoa

DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, DAKIKA 4 ZIMEONGEZWA

Dk 89, Dakika moja imesalia mpira kumalizika.
Dk 88, Rollers wanafanya mabadiliko, wanajaribu kupoteza muda.
Dk 86, Nsanjigwa ametolewa nje baada ya kuanza kubishana na Mwamuzi, ameenda jukwaani.Dk ya 85, Dakika 5 zimesalia mpira kumalizika, milango bado ni migumu.
Dk 83, Ajib anafanywa faulo, inapigwa sasa kuelekea Rollers, upande wa kulia mwa Uwanja

82, Rostand anafanya kazi kubwa leo, anaokoa krosi hapa, kona nyingine.
Dk 79, Chirwa anapata nafasi ya kupiga shuti, mpira unakwenda sentimita chache nje. Bado milango ni migumu.
Dk 78, Mchezaji Seko amedondoka chini, mpira umesimama.
Dk 75, Faulo, Chirwa anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.
Dk 74, Tayari ameshainuka, mpira unaendelea. Kwake Said Makapu, pasia huku pembeni kwa Ibrahim Ajibu. Bado Yanga wanao.Dk 73, Rostand ameumia tena, mpira umesimama.
Dk 72, Kinachoonekana hapa Rollers wanajaribu kupiga mashuti ya mbali kutafuta bao.
Dk 70, Chirwaaaaa, piga shuti moja engo ya kulia mwa Uwanja lakini linakuwa shuti mkaa.

Dk 70, Bado Rollers wameliandama vilivyo lango la Yanga.
Dk 68, Inapigwa, Dante anaokoa kwa Kicgwa, Yanga wanafanya mabadiliko. Yusuph Mhilu anatoka na Mwashiuya anachukua nafasi yake.
Dk 67, Kona nyingine inapigwa kuelekea Yanga
Dk 66, Mpira umeelemea kuelekea langoni mwa Yanga, Rollers wanashambulia vilivyo lango lao, matokeo bado ni 0-0.
Dk 65, Yanga wanarusha tena, Gadiel Michael, kwake Makapu, pigwa huku kwake Chirwa, wanaokoa huku Rollers.

Dk 63, Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Rollers, ni karibu na eneo la hatari la wapinzani, unarushwa huku, kwake Chirwa, unakwenda nje.
Dk 62, Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kamusoko, anaingia Ajibu
Dk 59, Yanga wanapandisha mashambulizi sasa lakini Rollers wanaokoa, wanakwenda langoni mwa Yanga, linapigwa shuti kali, Rostand anaokoa kwa kupiga shuti kueleka kwa wapinzani.
Dk 57, Yanga wanazidi kuruhusu lango kushambuliwa.
Dk ya 54, Inapigwa huku, kipa anadaka.
Dk 53, Hatariii, shuti kali linapigwa na mshambuliaji wa Rollers, Rostand anaupangua mpira na kutoka nje, kona.

Dk 52, Inapigwa faulo kati ya uwanja kuelelea Yanga, pigwa kulee, Rostand anaidaka.
Dk 51, Takribani dakika zote za kipindi cha kwanza Rollers wameliandama lango la Yanga.
Dak 49, Hatari langoni mwa Yanga ndani ya penati boksi, Rostand anaokoa.
Dk 48, Rollers wanapandisha mashambulizi, Gadiel Michael anatoa mpira, unarushwa kuelekea Yanga, unamkuta lemponye, anapiga, Dante anaokoa.
Dk 46, Mpira umesimama, mchezaji wa Township ameumia, unapigwa kuelekea Yanga
Dk 45, Yanga wanaanzisha, matokeo ni 0-0.

DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA PILI ZIMEANZA

DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA, MPIRA NI MAPUMZIKO

Dk 45, Matokeo ni 0-0 bado
Dk 44, Rollers wanakwenda sasa, wanashambulia kueleka lango la Yanga, wanapotezana hapa, Yondani anaokoa mpira na kupiga mbele.
Dk 43, Papy amelala chini, yawezekana akawa ameumia, madaktari wanaingia kumpa huduma.
Dk 42, Dakika 3 zimesalia mpira kwenda mapumziko
Dk 41, Hatari katika lango la Yanga, namna gani mshambuliaji huyu anakosa bao la wazi kabisa, matokeo nado ni 0-0.
Dk 39, Yondaaaaani, piga mashine moja inapaa juu ya lango la wapinzani.
Dk 38, Mechi bado ngumu, nyavu bado hazijatikisika hata kwa nje.
Dk 37, Rollers wanashambulia pembeni ya kulia mwa Uwanja, lakini mpira unatoka nje.
Dk 35, Mpira anao Rostand, anapiga mbele huku, Rollers wanatoa nje, unarushwa huku, Yanga wanautoa, kwake Lemponye, wanagongeana hapa, faulo.

Dk ya 34, Obrey Chirwa yupo chini, mpira umesimama, Lwandamina anajibizana na, Yondani anaingilia anapewa kadi ya njano.
Dk 33, Juma Abdul anautoa mpira nje, Rollers wanarusha, hatari katika eneo la Yanga ndani ya penati boksi, wanarudisha tena nyuma na kuanza upya.
Dk 32, Inapigwa unamkuta huku Mhilu, anapiga shuti lakini inakuwa goli kiki.
Dk 31, Mpira unarushwa kuelekea Yanga, Yanga wanauchukua, kwake Chirwa, faulo, inapigwa kuelekea Rollers.
Dk 30, Yondani na mpira, anapasia huku pembeni lakini Rollers wanauchukua, unapigwa mbele huku, Vincent anakataa anautoa nje.

Dk ya 28, Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kucheza faulo, inapigwaaa, hatari, Mwamuzi anasema offside.
Dk 27, Mpira sasa anao Kamusoko katikati mwa Uwanja, anapasia kwake Mhilu, namna gani ananyang'anywa na wapinzani.
Dk 24, Nyavu bado ni ngumu kutikisika kwa pande zote mbele, kila timu inafanya mashambulizi ya kushtukiza.
Dk 22, Youthe Rostand ameumia, anapeana tano na Mwamuzi, tayari ashainuka.

Dk 21, 0-0 mpaka sasa, kila timu inapambana kupata bao la mapema, Rollers wanakwenda, pigwa moja ndefuuu, inatoka, free kiki kuelekea Rollers.
Dk 19, Faulo inapigwa kuelekea Yanga, kushoto kidogo mwa Uwanja, inapigwa, beki Andrew Vincent anaokoa kwa kichwa.
Dk 18, Gadiel Michael anatoka nje kugagangwa, ameumia.
Dk 17, Yusuph Mhilu anaenda na mpira sasa, anaukokota na anauota mwenyewe, unarushwa kuelekea Yanga..

TUNAOMBA RADHI KUTOKANA NA MATANGAZO YA AZAM TV KUKATIKA, TUTAREJEA PALE WATAKAPOREJEA TENA HEWANI

Dk 5, Kapteni wa Township anapoteza pasi kati mwa uwanja baada ya kutenegezewa na mwenzake, mpira unakwenda. nje, Yanga wanarush.
Dk 5, Mpira umeanza kwa kasi, kila timu inajaribu kutafuta bao la mapema.
Dk 3, Township wanamiliki mpira eneo la kati, unapigwa kwenda mbele lakini unatok nje.
Dk 2; Dakika ya pili ya mchezo, mpira umeanza punde.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic