March 7, 2018


Na George Mganga

Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry SC kutoka Misri, umemalizika usiku huu katika uwanja wa taifa kwa matokeo ya 2-2.

Walikuwa ni Simba walioanza kuziona nyavu za Al Masry mapema tu katika dakika ya 10 kwa nja ya penati, baada ya beki wao kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Haikuchukua muda kwa Al Masry kusawazisha, kwani baada ya kufungwa bao la kwanza walianza mashambulizi makali langoni mwa Simba, na katika dakika ya 11, Ahmed alifunga bao la kusawazisha na kuufanya ubao wa matokeo uwe 1-1.

Mchezo huo ambao Al Masry waliutawala zaidi kipindi cha kwanza, mnamo dakika ya 26 tena walipata bao la pili kwa njia ya penati kupitia Abdalrauf, baada ya Erasto Nyoni kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza mwanzoni kwa Al Masry kuzidi kuonesha uhai, lakini baadaye Simba wakaanza kujibu mashambulizi wakilisakama lango la wapinzani wao, ambapo katika dakika ya 74, Emmanuel Okwi, aliweza kumlaza kwa chenga beki wa Al Masry na kuwa penati ambayo ilizaa bao la pili kwa Simba.

Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Simba SC 2-2 Al Masry SC.

3 COMMENTS:

  1. Simba pia ilitawala mchezo kipindi cha pili

    ReplyDelete
  2. Penalty ya pili ya Simba ilipatikanaje?

    ReplyDelete
  3. Almasry wamethibitisha kuwa ni timu imara kaliba ya Alhal na Zamaleki. Niwape heshima kubwa yakwamba wameutendea haki mpira kwani nilitarajia walikuja kupaki basi lakini badala yake walicheza mpira wao hasa. Kuna kitu kimoja ambacho inawezekana kabisa Almasry waliumwa sikio na baadhi ya watanzania kuwa Simba haikuwa vizuri sana kwenye ulinzi kitu amabacho kiliwapa Almasry kiburi na ujasiri wa kutoka na kwenda kushambulia kama vile wapo kwao. Ila cha kufarahisha zaidi licha ya Simba kutoa sare nyumbani wameonesha kuwa sio timu ya kubeza Africa na kama simba watatulia na kuendeleza level hii waliofikia sasa watanzania watarajie makubwa zaidi kutoka kwao siku za usoni. Wakati mwengine ni kitu cha kufurahia zaidi kwa timu zetu kupangwa na timu zenye viwango vikubwa Africa. Wamisri wanajua fika kuwa kwa simba kazi haijaisha kwa hivyo ni matarajio yetu kuona makocha wakiyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic