March 6, 2018



Dak ya 2, Mpira umeanza hivi punde, ubao unasomeka 0-0

Dak ya 2, Hassan Kessy anapiga shuti kali langoni mwa Rollars lakini mpira unatoka nje

Dak ya 3, Hatari, mshambuliaji wa Rollers anakosa bao la wazi hapa, matokeo ni 0-0

Dak ya 6, Wachezaji wa Township wanaanza nyuma huku taratibu kuelekea eneo la kati ya uwanja

Dak ya 6, Yanga wanauchukua na kupasiana pia eneo la kati, Chirwa anapata pasi kulia mwa Uwanja lakini mpira unatoka nje.

Dak ya 7, Rollars wanarusha mpira kuelekea lango la Yanga, ni baada ya kutolewa nje

Dak ya 8, Offside, Yanga wanapata kupitia Chirwa

Dak ya 8, Kessy anapasiana na Papy, Papy anampa tena Kessy, Kessy anapoteza wanachukua Township

Dak ya 9, Faulo inapigwa kuelekea lango la Yanga baada ya Sisikele kuchezewa faulo

Dak ya 10, Makapu anaokoa mpira uliopigwa langoni wa Yanga, Rollers wanauchukua tena na sasa wanapasiana eneo la hatari la Yanga.

Dak ya 10, Goooooo, Rollers wanapata bao la kwanza kupitia kwa Lemponye

Dak ya 17, Rollers wanaanza tena taratibu, Yanga wanauchukua, beki Isubo wa Rollers anaokoa

Dak ya 13, Hatarii katika lango la Yanga, Buswita anaokoa, ni kona

Dak ya 13, Inapigwaaa lakini kipa anaokoa

Dak ya 14, Mpira anao sasa Kabwili, Kabwili anampasia Makapu, Makapu anampasia Yondani

Dak ya 15, Hatariiii, linapigwa shuti kali na mshambuliaji wa Township lakini linagonga mwamba, ni hatari

Dak ya 17, Matokeo bado ni 1-0, Township wanaongoza, kipa Rostand anapasha, inawezekana aakachukua nafasi ya Kabwili

Dak ya 18, Hatari katika lango la Township, Tshishimbi anapiga shuti lakini linaenda nje, lilikuwa shuti kali

Dak ya 19, Chirwa sasa anakimbiza na kumuwekea Buswita lakini mabeki wanaokoa

Dak ya 20, Yanga 0-1 Township

Dak ya 20, Chirwa ameshika mpira eneo la hatari mwa Township na mpira unapigwa kuelekea Yanga

Dak ya 21, Yanga wanapata kona, anapiga lakini Chirwa anashindwa kuumudu, unatoka nje

Dak ya 22, Ajibu anapiga mbele lakini wapinzani wanakataa, unamfikia kipa wa Township na anaokoa

Dak ya 23, Yondan anafanyiwa faulo, mpira unalekezwa langoni mwa Yanga

Dak ya 23, Township Rollars wanaenda, inapigwa krosi finyu lakini Kabwili anadaka kiulaini kabisa

Dak ya 24, Yanga wanapasiana eneo nje kidogo ya 18 mwa wapinzani, Ajiiiiib, mpira unakwenda nje, Goli Kiki

Dak ya 26, Mpira unarushwa kuelekea lango la Yanga baada ya kutolewa nje

Dak ya 26, Rollers wanapasiana ndani ya 18 ya Yanga lakini mpira unaokolewa

Dak ya 28, Mpira sasa anao Tshishimbi, unaenda kwa Chirwa, Goli Kiki

Dak ya 28, Yondani anamtafuta Buswita, wananyang'anywa mpira, sasa wanao wapinzani

Dak ya 30, Goooooooo, ni Chirwaa, sasa ni 1-0, kazi nzuri ya Tshishimbi inaleta matunda

Dak ya 31, Ni kona sasa kuelekea Rollars, Yanga wanashambulia

Dak ya 32, Inapigwa lakini mabeki wanautoa nje, kona ya pili saa, anapiga inatolewa tena, ya 3 mfululizo.

Dak ya 32, Inapigwa tena, kunatokea hekaheka langoni kati ya kipa na mabeki lakini kipa anaudaka

Dak ya 34, Papy anaumiliki sasa mpira, anampasia Buswita lakini unatoka na kwenda nje

Dak ya 35, Rollars wanaumiliki mpira hapa, shuti linapigwa kuelekea langoni mwa Yanga lakini mpira unaokolewa

Dak ya 35, Gadiel anapiga krosi mkaa engo ya kushoto mwa Uwanja lakini mpira unakwenda nje

Dak ya 36, Yanga wanaanza lakini mpira unakwenda nje

Dak ya 37, Kabwili anaudaka mpira baada ya kupigwa shuti na mshambuliaji wa Rollars

Dak ya 37, Rollars wanajaribu kupata bao lakini Yanga wanaokoa

Dak ya 40, Matokeo ni 1-1, mpira umesimama kwa muda baada ya beki wa Rollars kuumia, sasa anangangwa

Dak ya 42, Yanga wanapata free kiki kulia mwa uwanja karibu na eneo la hatari la Rollars

Dak ya 43, Mpira umesimama tena, mchezaji wa Rollars ameumia

Da ya 44, Ajibu anapiga faulo, huku mchezaji aliyeumia akitoka nje, anapiga, kipa anaokoa inagonga mwamba, Offside

Dak ya 45,Dakika 2 zimeongezwa

Dak ya 46, Beki wa Rollars amemsukuma Yondan na mpira unakuwa faulo

Dak 45 zimekamilika, matokeo ni 1-1

Dak ya 53, Yanga wanapasiana eneo la kati mwa uwanja

Dak ya 54, Yanga wanapata kona, inapigwaaa, lakini mabeki wanaokoa, Tshishimbi anauchukua tena apige lakini mpira unakwenda nje

Dak ya 55, Kabwili sasa anaanza na mpira, anapiga kati huku lakini Yanga wanacheza faulo, mpira unapigwa kuelekea Rollars

Dak ya 56, Kessy anarusha mpira baada ya Rollers kuutoa, 

Dak ya 56, Tshishimbi anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi nahodha wa Township

Dak ya 57, Yanga wanaanza tena nyma, Makapu anapiga shuti ambalo kipa wa Rollers anadaka. Mpaka sasa Yanga wanajitahidi kupenya ngome ya Rollers lakini inakuwa ngumu

Dak ya 59, Mshambuliaji wa Rollers anapiga krosi mkaa na washindwa kuitumia vema, inatoka nje

Dak ya 59, Inapigwa krosi kali langoni mwa Yanga, inapigwa kichwa na mshambuliaji lakini inadunda chini na kupaa juu ya nyavu za Yanga, ilikuwa hatari

Dak ya 61, Matokeo bado ni 1-1

Dak ya 62, Hatari katika lango la Rollers, inapiwa krosi na gadiel Michael lakini inatoka nje

Dak ya 62, Mpira anao Yondan sasa, anampasia Gadiel, gadiel anaukokota kuelekea mbele lakini anababatizwa na mpinzani wake na mpira unakwenda nje

Dak ya 63, Buswiiita, mpira unakwenda nje

Dak ya 64, Hassan Kessy anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, Mwashiuya anapasha nje ya dimba

Dak ya 65, Yanga wanapata free kiki eneo la hatari langoni mwa wapinzani, ikitumika vema itaweza kuzaa bao, anaonekana Kessy, Ajibu wakitaka kupiga

Dak ya 66, Anapiga Ajiiibu lakini mpira unawababatiza mabeki na unatoka nje

Dak ya 68, Ameingia Mwashiuya kuchukua nafasi ya Ajibu

Dak ya 71, Bado ubao wa matokeo unasomeka ni 1-1

Dak ya 72, Mahadhi sasa anaenda na mpira kulia mwa uwanja, anapiga krosi, inakwenda nje

Dak ya 72, Mwashiuya anatoa nje, mpira unarushwa kuelekea Yanga

Dak ya 73, Yanga wanapasiana nyuma, Kabwili anao, anapiga mbele unaendaaa mpaka kwa kipa wa Rollars

Dak ya 75, Dakika 15 zimesalia mpira umalizike

Dak ya 77, Mwashiuya anapiga kona kuelekea lango la Rollers, ni kona ya 8 kwa Yanga, anapiga lakini mabeki wa Rollers wanaokoa

Dak ya 79, Yanga wanapata free kiki, anapiga Mwashiuya, anapigaaa, kipa anadaka taratibu kabisa

Dak ya 80, Matokeo ni 1-1 mpaka sasa, mchezo unaendelea

Dak ya 83, Goooooli Rollers wanapata bao la pili kupitia kwa Sikele

Dak ya 84, Matokeo sasa ni 2-1, Township wanaongoza

Dak ya 87 sasa, Rollers wanamiliki zaidi mpira, Kabwili anaanza, kwakwe Mwashiuya, anapiga krooosi, kona

Dak ya 88, Mwashiuya anapiga kona lakini mpira unatoka nje, ni goli kiki

Dak ya 90, Yanga 1-2 Township Rollers

Dak ya 92, Dakika 3 ziliongezwa, sekunde kadhaa sasa mpira uishe

Full Time, mpira umekwisha, Yanga inapoteza nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

1 COMMENTS:

  1. Yanga wanaichezea bahati ya kucheza katika makundi nafasi kama hizi uwa azijitokezi hadi baada ya miaka 20

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic