March 8, 2018





Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, imeelezwa kuwa hali ya kiafya ya Rais wa Simba, Evans Aveva ni mbaya.

Mahakama hiyo imeelezwa, Aveva amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Kutokana na hali hiyo, Aveva ameshindwa kuhudhuria tena mahakamani katika kesi yake utakatishaji fedha inayomkabili kwa mara ya sita mfululizo kutokana na juzi hali yake kubadilika ghafla akiwa mahabusu katika Gereza la Keko na kukimbizwa kwenye hospitalini hapo na kulazwa kwenye kitengo hicho kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Pamoja na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu;, Aveva anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.

Katika kesi hiyo ambayo iliitwa kwa ajili ya kutajwa jana  mbele ya  Hakimu Mkazi wa Makahama  ya Kisutu, Wilbad Mashauri badala ya  Victoria Nongwa ambeye hakuwepo ambapo mwendesha mashitaka mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru), Leonard Swai aliieleza mahakama kuwa  jadala kasi hiyo bado halijarudi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyengine huku akisema Aveva ameshindwa kufika kwa kuwa ni mgonjwa.

Wakili wa upande wa utetezi, Evodius Mtawala alieleza mahakama kuwa juzi  Jumatano walipokea taarifa kuwa mteja wao wa kwanza katika kesi hiyo (Aveva) hali yake  ni mbaya na amerudishwa Muhimbili katika kitengo cha wagonjwa mahututi hivyo ameshindwa kutokea.

"Mheshimiwa hakimu jana (juzi)  tulipata taarifa kwamba mteja wetu, Aveva hali yake ilibadilika ghafla hivyo amerudishwa Muhimbili na amelazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi hivyo ameshindwa kufika.

"Lakini nje ya hapo nikuweke sawa katika kumbukumbu kwa kuwa kesi inasimamiwa na hakimu mwengine kwamba ni muda jalada limekuwa lipo kwa DPP na kila tukija hakuna kinachoendelea cha maana hivyo tunaomba tuwape wenzetu Takukuru siku 14 ili wakija waje na kitu cha maana ambacho kitatoa mwanga kuliko kubakia kwenye siku saba ambazo zimekuwa hazina faida yoyote," alisema Mtawala.

Hoja hiyo iliweza kukubaliwa na pande zote mbili ambapo hakimu Mashauri alisogeza mbele kesi hiyo hadi  Machi 22, mwaka huu. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic