MAJIMAJI SASA YAHITAJI DAKTARI ILI KUTIBU MATATIZO YAO SUGU, KUMBUKA IPO MKIANI KWENYE LIGI
Na George Mganga
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Ruvuma, Golden Sanga, amesema hali ya Majimaji imeyumba hivi sasa na hawana uhakika wa kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi.
Sanga ameeleza kuwa hivi sasa hawako vizuri kifedha, jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa matokeo mazuri ndani ya timu yao ambayo ipo mwisho mwa msimamo wa ligi.
Aidha Sanga amesema timu haijasimama vizuri kutokana na baadhi ya wachezaji kusimamishwa ambao hawajatajwa na sababu za kusimamishwa kwao hazijawekwa wazi.
Vilevile, Mwenyekiti huyo ameweka wazi suala la kutokuwa na maelewano kwa baina ya viongozi klabuni, suala ambalo amedai linakuwa pia sababu ya kuendelea kukalia mkia katika msimamo wa ligi.
Uwepo wa changamoto hizo, umemlazimu Sanga kusema wanahitaji madaktari ili aweze kuwasaidia kuyatibu kwa maana yamekuwa sugu sasa.
Majimaji itaingia Uwanjani 'Sabasaba Stadium' ikiwa na alama 15 tu, kucheza dhidi ya Lipuli FC kutoka Iringa.
Source: E Sports, EFM
0 COMMENTS:
Post a Comment