March 12, 2018


Kagera Sugar itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kesho Jumanne.

Kagera itawakaribisha Mwadui kutoka Shinyanga ikiwa kwenye wakati mgumu wa kujikomboa kushuka Daraja.

Walima miwa hao wa Kagera hadi sasa wana tofauti ya pointi mbili na Mwadui FC walio nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi huku Kagera wakishika namba 14.

Kocha Meck Maxime atakuwa anatumia faida ya Uwanja wake wa nyumbani, Kaitaba Stadium, kujaribu kuinusuru timu yake iondoke kwenye hatari ya kuelekea Ligi Daraja la Kwanza.

Kiujumla timu zote mbili hazina maendeleo mazuri kwenye ligi msimu huu, ukiangalia zina tofauti ya pointi mbili tu, Mwadui ana 20 na Kagera ana 18, hivyo mmojawapo akipata matokeo, atakuwa amejitengenezea njia ya kukwepa kushuka chini.

1 COMMENTS:

  1. Kagera atashuka kweli....tatizo la Maxime anakamia baadhi ya timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic