March 28, 2018



Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana, Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema wapinzani walikuwa wazito.

Mayanga ameeleza kuwa mchezo huo ulikuwa vizuri kutokana na vijana wake kuonesha nidhamu na kuwa imara zaidi kwenye safu ya ulinzi, kitu ambacho kilipelekea wapinzani washindwe kupata bao.

Aidha, Mayanga amesema Congo walishindwa kuisumbua Stars kutokana na kuwa wazito miguuni na kuwapa faida Stars kupata mabao hayo mawili.

Stars ilifunga mabao yake kipindi cha pili baada ya kile cha kwanza kwenda suluhu ya 0-0  kupitia kwa Mbwana Samatta na Shiza Ramadhan Kichuya.

Stars ilipata ushindi huo ikiwa imetoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1 huko Algiers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic