Huku mambo yakizidi kuiendea kombo katika Ligi Kuu Bara huku wakiwa nafasi ya 12, uongozi wa Mbao FC ya Mwanza umeibuka na kusema kuwa wao hawana tatizo bali waamuzi ndiyo wanawaonea.
Mbao ambayo inanolewa na Kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije, leo Jumatano itacheza na Mbeya City mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja Sokoine jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Zephania Njashi, alisema vijana wapo vizuri na wamejiandaa vizuri kwani wamepoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Prisons.
“Tumejiandaa vizuri kuhusu mchezo wetu wa kesho (leo) na vijana wote wapo fiti hakuna majeruhi hata moja, sisi hatuna tatizo lolote kwani waamuzi ndiyo wanatukandamiza unakuta wapinzani wanapewa penalti ambayo siyo ya halali kabisa.
“Lakini sisi tunaenda nyumbani kujipanga zaidi na tunaanza na Mbeya City kisha tunajiandaa kucheza na Azam baada ya hapo mechi zetu zote zitakuwa nyumbani hivyo tunajipanga kuhakikisha tunashinda,” alisema Njashi.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment