NGORONGORO HEROES WAANZA KUWAWINDA DR CONGO KUELEKEA KUFUZU AFCON 2019
Na George Mganga
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imeanza mazoezi leo Jumatano Machi 7, 2018 kwenye Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Ngorongoro wameanza mazoezi hayo kujiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya DR Congo utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo inataraji kupigwa Machi 30 dhidi ya DR Congo na baadaye mchezo wa marudiano utachezwa April 22 2018.
Michuano hiyo ya AFCON chini ya miaka 20, itafanyika Nigeria mwaka 2019.
0 COMMENTS:
Post a Comment