March 7, 2018

BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA KATIKA MOJA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA WAKIWA WAMEPENDEZA KATIKA JEZI ZA TIMU HIYO UKIACHANA NA WALE WAPUUZI WACHACHE WALIOKWENDA KUJIPENDEKEZA NA KUOMBA JEZI ZA WAARABU WA AL MASRY.


Hii ni sura mbaya na ya kushangaza.

Juzi Jumatatu, baadhi ya makomandoo wa Yanga na mashabiki waliamua kuvamia mazoezi ya Al Masry na kuomba jezi ili waweze kuishangilia timu hiyo katika mchezo wa dhidi ya Simba, huku wakisikika wakisema ‘Simba 1 Al Masry 3’.

Katika mchezo huo ambao unapigwa leo Jumatano saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, makomandoo hao hawakusita kuonyesha ushabiki wao kwa timu hiyo wakati wakifanya mazoezi juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku wakilitaja jina la mshambuliaji wa timu hiyo,  Aristide Bance raia wa Burkinafaso.

Makomandoo hao walifika uwanjani hapo kuangalia mazoezi ya wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Township Rollers kabla ya  mchezo wao uliopigwa jana kwenye Uwanja wa huo ambapo timu hiyo ilipomaliza mazoezi na kuwapisha Al Masry, wao walikomaa na kuwafuata viongozi ili wawape jezi watakavaa leo na kuwashangilia.

Tuliwashuhusia makomandoo hao wakijadiliana kuwaomba jezi viongozi hao  kabla ya kuwafuata  lakini hawakuweza kufanikiwa kwa kuwa wajibiwa kuwa:” Mtatusamehe, hatujabeba jezi za kutosha.”


“Lazima Simba itafungwa mabao 3-1, nawahakikishia na wale msiwe na hofu hata kidogo,” alisema shabiki mmoja akiwa amevaa jezi ya Yanga wakati anahojiwa na kituo kwa One Sport cha Misri.

SOURCE: CHAMPIONI

6 COMMENTS:

  1. Ila sura nzuri ni hii iliyoonyeshwa na mashabiki wa Simba kuishangilia Township rollers hadi timu hiyo ikaenda kutoa shukrani kwa mashabiki wa Simba mara baada ya mechi kwisha aibu kubwa hiyooo. Kwa tabia hii Tanzania itabaki na aibu kuu kimataifa maana timu ngeni zitakuja bila mashabiki kwani mashabiki zitawakuta huku huku tena wakutosha. Faida ya kucheza nyumbani haitakuwepo kabisaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni hapo juu amabae ni shabiki wa Yanga unachokisema hakieleweki yaani pumba kabisa. Unaambiwa mashabiki wa Yanga walikwenda kujipendekeza kuomba jezi na kuwapa sapota Almasry mazoezini yaani makomandoo mashabiki wa Yanga vihere vihere vilivyo wajaa kusubiri mechi ichezwe ndio wawashangilie hao Almasry wameona wanachelewa ujinga mtupu. Sasa kwanini mashabiki wa Simba wasijibu mapigo wakati mwengine ujinga ujinga tu? Sina haja ya kuinguza siasa lakini utaona jinsi gani Magufuli anavyoteseka kuwaongoza Watanzania. Sisi Watanzania ni watu wa hovyo kabisa tusiojitambua.

    ReplyDelete
  3. Tuna kazi kubwa ya kuelimishana juu ya utaifa wetu, umoja wetu na hivyo uzalendo wetu. Sisi ni wamoja mbele ya timu pinzani za nje. Tunapaswa kushabikia timu zetu za ndani - iwe Simba, Yanga, Azam, Singida, Majimaji, mradi ni timu ya Tanzania inawakilisha nchi yetu dhidi ya timu ya nje, basi busara inatutaka tushabikie timu yetu ya nchi yetu - TANZANIA.

    ReplyDelete
  4. Mimi nipo huku nje waarabu wanatucheka na kutushangaa kwa kutuona watu wa ajabu tusiokua na uzalendo wa nchi yetu na hii si kwa yanga bali simba mechi ya jana na pia mechi zilizopita walishangilia timu za wageni na kuacha kushangilia timu za nchi yao !!! Huu ni ulimbukeni na viongozi lazima wawaelimishe wapenzi wa michezo katika hili maana ni suala la mda mrefu na halijapatiwa suluhisho!!

    ReplyDelete
  5. Saleh Jembe acha ufala

    ReplyDelete
  6. Wajenge viwanja vyao nadhan hili la kuzomea uwanjan litapona

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic