March 13, 2018


Na George Mganga

Mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara unataraji kuendelea jioni ya leo katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera

Kagera Sugar itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja huo ikiikaribisha Mwadui FC, mechi ambayo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Kiwango cha Kagera msimu huu hakijawa kizuri kutokana na timu hiyo ipo kwenye harakati za kuepuka kushuka daraja.

Akihojiwa na Chombo cha Habari, EFM Radio, Kocha wa Maxime, amesema wao wamejipanga na watajua namna gani ya kupata matokeo kwenye mchezo  wa leo.

"Tunajua namna ipi tumejipanga, iwe kinyumenyume ama kimbelembele, tutapambana" alisema.

Timu hiyo ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo ikiwa na pointi 18.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic