Na George Mganga
Mehi ya Ligi Kuu bara kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Mbao FC, iliyokuwa inapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya imeshindwa kumalizika.
Sababu za kushindwa kumalizika kwa mcheza huo ni baada ya mvua kubwa kuendelea wakati pambano hilo likiendelea huku Prisons wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Prisons walipata bao la kwanza kwa njia ya penati, lililofungwa na Mohammed Rashid katika dakika ya 11, na mpaka wanakwenda mapumziko, Prisons walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Baada ya kuanza kipindi cha pili, ilichukua takriban dakika 5 pekee, ambapo katika dakika ya 50 mvua ilizidi na kusababisha Mwamuzi wa mchezo huo kusimamisha mpira.
Dakika zilizosalia katika mchezo huo, zitamaliziwa mapema kesho asubuhi ili kupata mshindi halali wa mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment