March 3, 2018


Na George Mganga

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka (TBPL), imemsimamisha kwa muda mlinda mlango wa Azam FC, Razak Abalora, kutoitumikia timu hiyo.

Abalora amesimamishwa kutoka na makosa ya kumtupia lawama Mwamuzi Jonesia Rukiya, baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, uliochezwa Februari 7, 2018 katika uwanja wa taifa.

Adhabu hiyo itadumu mpaka pale suala lake litakapojadiliwa na Kamati ya Nidhamu kuhusiana na makosa yake ya kumlalamikia Mwamuzi kuwa aliwanyima penati walipokutana na Simba,

Kipa huyo hataweza kuichezea Azam katika mchezo wa leo dhidi ya Singida United, itakayopigwa Azam Complex, jioni ya leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic