March 25, 2018



Baada ya Taifa Stars kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria wiki hii, Naibu Meya wa jiji la Mwanza, Mh. Bhiku Kotecha, ametoa ushauri kwa timu hiyo.

Stars ilikubali kichapo cha jumla ya mabao manne kwa moja ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Julai 5 Algeria.

Kotecha ameutaka uongozi wa timu hiyo chini ya Mkuu wa Benchi la Ufundi, Salum Mayanga, kufanya maandalizi ya muda mrefu ili kuwafanya wachezaji waweze kuzoeana kabla ya mechi.

Naibu huyo ameshauri ni vizuri timu hiyo ikawa inaweka kambi ya muda mrefu ili kupata muunganiko mzuri wa wachezaji ili kikosi kiweze kuleta matokeo chanya Uwanjani.

Stars ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo utakaopigwa keshokutwa Jumanne, Machi 27 2018.

CHANZO: RADIO ONE

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic